Bongo Flava Mzuka
Kama
wewe ni msela wa muziki wenye miporomoko ya reggae/ragga na mixa zingine za muziki kama zouk,afrikan Jazz. Je umeshawahi kumsikia kwenye bomba au kumtia machoni jukwaani Mani au Ras Nas au Nasibu Mwanukuzi. Ras Nas ni mbongo anayefanya shughulii zake za muziki uzunguni nchini Norway ndani ya Oslo.
Jambo
moja ambalo pengine masela na mashabiki wake hawajui ni kuwa Ras Nas au Mani Nas
ni mwanasheria kitaaluma. Alipiga buku sheria katika chuo kikuu cha
Dar-es-salaam. Anaweza kutunga na kudodondosha mashairi hatari... usipime!!