Produza atutoka

Producer(mtunzi) makini wa muziki nchini aliyejulikana kwa jina la kisanii Roy Bukuku aka Roy wa G Records, amefariki dunia jana(08-10-2008). Kijana mwenzetu hatunaye tena baada ya kusumbuliwa homa ya mapafu huko Mkoani Mbeya.


Roy ni producer mwenye kipajikutoka studio za G2 Records, alijishughulisha na nyimbo kali ya Vailet ya Mtonya na nyinginezo zaidi.

Hata hivyo alikua na kipaji cha kupiga kinanda(PIANO). Ambapo mnamo mwaka 1985 akiwa nchini Uingereza alishiriki mashindano ya kupiga chombo aina ya piano na kuibuka mshindi na kujinyakulia tuzo iliotambulika kwa jina la SEVEN OAKS THREE ARTIST FESTIVAL.

Pamoja na ujuzi wa muziki Roy pia alikuwa mtaalamu wa mambo ya Kompyuta, Graphics.

Kwa kweli tumepata pigo kubwa sana, Roy tutakukumbuka daima.