Type in Your Email
AMINA CHIFUPA AFARIKI DUNIA
Muheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum Amina Chifupa,umri wa miaka 26, ametutoka duniani mda wa saa 2.45 usiku katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi Lugalo, Dar es Salaam.

Source: damija
Mbunge Amina amefariki kutokana na kuugua si kwa muda mrefu, Malaria na kisukari, magonjwa hayo yalijitokeza siku kadhaa kwa muda mchache kabla ya kujiandaa na kikao cha Bunge cha Bajeti kuu ya Tanzania.
Mzee Mohamed Mpakanjia, ambaye pia ni mume wake mpendwa alithibitisha kuwa kifo cha kusikitisha na kutaarifu utaratibu unafanywa wa kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Njombe, mkoa wa IRINGA kwaajili ya mazishi yatakayofanyika kesho.
Mbunge Chifupa aliweza kupata umaarufu wa kuwa Mbunge kijana na mdogo ki umri kutinga bungeni kwa haadhi ya vijana na alijitahidi kutikisa Bunge kwa kuwa kipao mbele katika harakati za kuwamata wauza na watumiaji wa madawa ya kulevya(BANGI na KOKAIN).
Ndani ya miezi 18 alishikilia bango msemo wake wa kutetea vijana, kupunguza rushwa na pia elimu kwa watu wote.
Kabla ya hapo alikuwa ni mtangazaji maarufu wa redio ya Clouds FM.
Amina, 20/5/1981 na kuhudhuria shule ya msingi ya Ushindi na baadaye kujiunga na shule ya sekondari Kisutu, aljiunga pia na shule ya sekondari ya Makongo, alikomaliza kidato cha sita mwaka 2001.
Watuhodari tunapenda kujiunga na msiba huu mkubwa kwa vijana na watu wanaopenda maendeleo ya vijana nchini Tanzania, Tumuombe Mungu amlaze Mheshimiwa Mbunge Amina Chifupa roho yake mahali pema peponi.