Type in Your Email
WEZI WA EPA CHOKA MBAYA

Aliongeza kua licha ya kuzuiwa hata kwa magari ya kifahari wanayomiliki vigogo hao, pasipoti zao za kusafiria pia zimezuiliwa ili wasikimbilie nje ya nchi. Licha ya hatua hiyo, Rais Kikwete alisema ameiagiza Benki Kuu (BoT) kufunga akaunti hiyo ambayo kwa mujibu wake ina zaidi ya Sh bilioni 130 na fedha hizo
ziwekwe katika mfuko mkuu wa serikali.
“Ikitokea mtu ajitokeze kudai (kutokana na EPA) tutamlipa,” alitamka Rais na kuiamrisha serikali kugawanya fedha kila mwaka kwa ajili ya dharura ya malipo kama hayo. Aliwasisitizia wananchi kufahamu kwamba fedha hizo si za umma, ni za watu wa nje ambao hawakupelekewa fedha zao.
Pia ameagiza kwamba fedha zitakapopelekwa serikalini baadhi zitumike kuongeza ruzuku ya mbolea na dawa za mifugo.
Alitamka pia, fedha nyingine zitahifadhiwa katika Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) zitumike kutoa mikopo ya kilimo na kama sehemu ya mchakato wa kuanzisha
benki ya kilimo.